Turning Point ni mradi wa kutokomeza umaskini wenye awamu tatu, unaolenga mabadiliko yanayoonekana ya maisha ya wengi wa watu wasio na fursa mijini na vijijini.
Kwa kuungana na wana maendeleo wenzetu wa kitaifa na kimataifa, mradi wa THIG wa Turning Point unalenga hasa kwenye kuleta huduma bora za kiafaya karibu zaidi na watoto pamoja na familia zisizo na fursa hizo, kurekebisha makazi, kutengeneza ajira, kukuza nishati rafiki kwa mazingira na utunzanji wake, kuboresha usafi, usimamiaji taka, utafiti na upatikanaji rahisi wa taarifa.