Incubation Hub (i-Hub) ni uvumbuzi mahiri na wenye ari ya kiteknolojia unaolenga kutengeneza maelefu ya ajira na fursa endelevu za kibiashara kwaajili ya watu barani Afrika kupitia utekelezwaji wa mipango ya kijasiriamali maalum kwa jamii.
Kipindi cha awamu ya kwanza ya i-Hub, THIG pamoja na wadau mbali mbali, wanalenga kutengeneza ufanisi na fursa zinazoshikikika kwaajili ya watu mbalimbali, tukilenga hasa katika sekta ya Kilimo, Usafirishaji, Mali zisizo hamishika (Real Estate) na Mitindo.
i-Hub inavuvia ukuaji endelevu na wenye faida kwenye uwekezaji wa kilimo katika miji na vijiji barani Afrika kupitia juhudi za uhusiano wa kiteknolojia wa hapo kwa hapo kati ya wakulima, wamiliki ardhi, wataalamu wa kilimo, wagawaji pembejeo, wasimamizi wa miradi, vibarua, wasafirishaji, wasambazaji, mawakala wa mauzo, mawakala wa uuzaji bidhaa nje pamoja na SME za sekta ya kilimo.