Karibu Jamii

Jamii” ni neno la kiswahili, ni bidhaa ya kijamii ya kiuwekezaji, iliyoundwa na timu ya THIG kwa ajili ya fursa mbadala ya kujipatia kipato “Kipato Mbadala”..

Ni gari la kukodisha, teksi, inayokupa fursa ya biashara ya pamoja kwenye sekta ya usafiri, ila kwa wakati huu unamiliki gari kwa kushirikiana na wengine, kugawana mapato, kusafiri pamoja, na kuunda fursa za ajira katika Jamii za Kiafrika.

Kwa sasa hatumiliki App ya usafiri, magari yamesajiliwa na makampuni yanayo ongoza nchini zenye App zinazo simamia teksi na watoa huduma za teksi, kama vile kampuni ya Uber, Bolt (taxify), n.k.

Jamii ni moja wapo ya mipango ya i-Hub ya kujiongezea kipato kutoka katika sekta ya usafirishaji, iliyoundwa kwa maendeleo endelevu kwa lengo la kuongeza usawa wa mapato katika nchi za Kiafrika. Kutokana na ukuaji wa haraka wa uhamiaji kutoka vijijini kuja mijini barani Afrika na shauku ya kupata huduma mbali mbali bora, hii inaleta fursa ya kutoa huduma bora za usafiri na ya uhakika katika jamii zetu za Kiafrika.

Tuna shauku kubwa ya kutimiza ahadi zetu, kama inavyotajwa kwenye ukurasa wetu wa mradi wa i-Hub, Incubation Hub (i-Hub) ni uvumbuzi mahiri na wenye ari ya kiteknolojia unaolenga kutengeneza maelefu ya ajira na fursa endelevu za kibiashara kwaajili ya watu barani Afrika kupitia utekelezwaji wa mipango ya kijasiriamali maalum kwa jamii.

Nunua gawio kwenye teksi na ujipatie kipato kila mwezi

Jiunge na Jamii leo.

Msaada? Ongea Nasi